Uchaguzi wa NOC-K wasitishwa na Mahakama Kuu ya Eldoret

Jaji Nyakundi alitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kusema itasikizwa tarehe 23 mwezi huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uchaguzi wa kamati ya Olimpiki nchini NOC-K, uliokuwa umesubiriwa kwa hamu ghamu umekosa kufanyika leo baada ya Mahakama Kuu ya Eldoret kusimamisha zoezi hilo .

Hii ni kufuatia kesi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa Triathlon Joyceline Nyambura, ya kupinga kufungiwa nje ya uchaguzi huo kinyume cha sharia za NOC-K.

Jaji Nyakundi alitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kusema itasikizwa tarehe 23 mwezi huu.

Ni mara ya pili kwa uchaguzi huo kuahirishwa baada ya kuahirishwa tena Aprili 24, baada ya mashirikisho manne ya michezo kukosa kukubaliana kuhusu wapiga kura wao.

Katibu Mkuu wa NOC-K Francis Mutuku ametaja kuwa kinachoshuhudiwa ka tika uchaguzi wa kamati hiyo ni ubabe wa kisiasa.

Hata hivyo kambi inayoongozwa na Naibu Rais wa kwanza Shadrack Maluki, imemshutumu jaji wa mahakama ya kutatua migogoro michezoni SDT ,Allan Mola, kwa kuonyesha mapendeleo kwenye kesi zilizowasilishwa .

Share This Article