Uchaguzi wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki nchini NOC, ulioratibiwa kuandaliwa leo huenda ukacheleweshwa au kukosa kuandaliwa leo, baada ya mahakama ya kutatua migogoro ya michezo nchini- SDT, kutoa amri ya kusitisha zoezi hilo.
SDT ilisema jana jioni kuwa ajenda nyingine za mkutano mkuu wa AGM zitaendelea isipokuwa tu uchaguzi wa viongozi.
Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na mashirikisho ya michezo 14 dhidi ya Kamati ya Olimpiki, Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC na msimamizi wa uchaguzi huo.
Uchaguzi wa NOC ambao umezua mhemko mkubwa ulitarajiwa kuandaliwa leo huku waaniaji wa nyadhfa mbalimbali wakigawana kwa kambi mbili.
Mashirikisho ya michezo 25 yaliyoidhinishwa pamoja na maafisa wanne wa kamati kuu ya NOC, wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa viongozi watakaohudumu afisini kwa miaka mine ijayo.
Naibu wa kwanza wa Rais Shadrack Maluki, wanapambana na Kaibu Mkuu Francis Mutuku, kutaka kumrithi Paul Tergat, ambaye muda wake wa kuhudumu wa miaka minane umekamilika.