Tuzo za mwaka huu za wachezaji bora barani Afrika zitaandaliwa nchini Morocco tarehe 19 mwezi huu.
Itakuwa mwaka wa tatu mtawalia kwa hafla hizo kufanyika nchini Morocco baada ya mji wa Marrakech kuandaa Makala ya mwaka 2023 na 2024.
Vitengo vitano vya mchezaji bora kwa wanaume na wanawake, kocha bora kwa wanaume na wanawake, mchezaji bora wa nyumbani kwa wanaume na wanawake, klabu bora ya mwaka kwa wanaume na wanawake, timu bora ya mwaka kwa wanaume na wanawake na mchezaji chipukizi bora wa mwaka.
Baadhi ya wanandinga wanaowania tuzo ya mchezaji bora kwa wanaume ni pamoja na Achraf Hakimi wa PSG na Morocco, Mo Salah wa Liverpool na Misri, Victor Osimhen wa Nigeria na Galatasaray, Serhou Guirassy kutoka Guinea na Borussia Dortmund, Denis Bouanga wa Gabon na Zambo Anguissa wa Cameroon na Napoli.