Tusker FC yamsajili mlinzi Eugene Ikutwa  kutoka Bidco United

Ikutwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Tusker wanapoiandaa kwa msimu uajo baada ya kiungo Vincent Owino.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu  ya Tusker FC imekamilisha usajili wa mlinzi wa pembeni kulia Eugene Ikutwa  kutoka klabu ya Bidco United.

Ikutwa aliye na umri wa miaka 22,amesaini mkataba wa miaka miwili akitarajiwa kuisaidia Tusker kuimarisha safu yao ya nyuma msimu ujao wa Ligi Kuu.

Kocha mkuu wa Tusker FC Charles Okere amemsifia mlinzi huyo akiwa na Imani kuwa atawasaidia kuziba  mapengo ya safu ya ulinzi yaliyowaponza msimu jana.

Ikutwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Tusker wanapoiandaa kwa msimu uajo baada ya kiungo Vincent Owino.

Share This Article