Tuko tayari kuandaa CHAN,asema Waziri Mvurya

Kenya, itaandaa fainali za CHAN na AFCON, pamoja na majirani Uganda na  Tanzania.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, amekariri kuwa Kenya iko tayari kuandaa fainali za  nane za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaosakata soka katika ligi za nyumbani almaarufu CHAN.

Mvurya amesema wameanza mchakato wa kuaindaa timu ya taifa Harambee Stars kwa fainali za CHAN na kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.

Kenya, itaandaa fainali za CHAN na AFCON, pamoja na majirani Uganda na  Tanzania.

Waziri ametoa changamoto kwa Harambee Stars kutwaa Kombe la CHAN kama maandalizi ya AFCON.

Fainali za CHAN zitaandaliwa kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

TAGGED:
Share This Article