Tuju ajiuzulu kutoka Jubilee

Waziri huyo wa zamani amesema hajaelewa mwelekeo wa chama cha Jubilee katika kipindi cha majuma sita amekuwa nje ya nchi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa zamani Raphael Tuju ametangaza kujiuzulu kutoka chama cha Jubilee.

Kwenye waraka kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Tuju ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho,  amesema haoni thamani  yake kwa chama cha Jubilee  kwa sasa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa yuko radhi kufanya kazi na Rais mstaafu siku za usoni.

Waziri huyo wa zamani amesema hajaelewa mwelekeo wa chama cha Jubilee katika kipindi cha majuma sita amekuwa nje ya nchi.

Share This Article