Timu ya Kenya ya mita 100 kwa wanariadha wanne wanaume yafuzu kwa mashindano ya Dunia

Kikosi cha Kenya kilichowajumuisha Boniface Mweresa,Ferdinand Omanyala,Meshack Babu, na Steve Odhiambo, ilimaliza ya pili kwenye mchujo wa Jumapili mjini Guanzhou ,China kwa muda wa sekunde 38.51.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya mita 100 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti wanaume imejikatia tiketi kwa mashindano ya Riadha duniani Septemba mwaka huu mjini Tokyo,Japan.

Kikosi cha Kenya kilichowajumuisha Boniface Mweresa,Ferdinand Omanyala,Meshack Babu, na Steve Odhiambo, ilimaliza ya pili kwenye mchujo wa Jumapili mjini Guanzhou ,China kwa muda wa sekunde 38.51.

Kwa jumla timu tatu za Kenya  za mita 100 wanaume ,mita 400 wanaume na mita 400 mseto zimefuzu kwa mashindano ya dunia yatakayoandaliwa Tokyo, Japan, Septemba mwaka huu.

Mbio za Dunia za kupokezana kijiti ziatakamilika leo nchini China.

Share This Article