Majaribio ya kitaifa kuchagua kikosi cha Kenya kwa mashindano ya Riadha Ulimwenguni yataandaliwa keso Jumanne katika uwanja wa Ulinzi Complex.
Wanariadha 150 waliotimiza muda na masharti ya kufuzu wamealikwa kwa majaribio hayo.
Mabingwa watetezi Faith Kipyegon katika mita 1500 na 5000, pamoja na Mary Moraa mita 800, wamepewa tiketi ya moja kwa moja baada ya kutwaa dhahabu mwaka 2023 mjini Budapest,Hungary.
Pia Beatrice Chebet,Margaret Akidor,na Agnes Jebet Ng’etich tayari wamefuzu kwa mita 5000, pamoja na Edwin Kurgat,Ishmael Kipkurui na Benson Kiplangat, ambao waliwahi tiketi za mita 10,000 wanaume.
Makala ya 20 ya mbio za Riadha Ulimwenguni zitaandaliwa kati ya Septemba 13 na 20 mwaka huu mjini Tokyo Japan.