Timothy na Reynold Cheruiyot wafuzu kwa fainali ya mita 1500, Tokyo

Upande wake, Reynold aliongoza mchujo wa pili kwa muda wa dakika 3 sekunde 36.64 na kufuzu kwa fainali ya Jumatano.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Dunia wa mita 1500 mwaka 2019 Timothy Cheruiyot na bingwa wa dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 Reynold Cheruiyot wamejikatia tiketi kwa fainali ya mashindano ya Riadha Uimwenguni jijini Tokyo, Japani.

Cheruiyot alifuzu kwa fainali baada ya kumaliza wa nne katika nusu fainali ya kwanza  leo Jumatatu akitimka kwa muda wa dakika 3 sekunde 35 .61.

Upande wake, Reynold aliongoza mchujo wa pili kwa muda wa dakika 3 sekunde 36.64 na kufuzu kwa fainali ya Jumatano.

Awali, leo pia, Wiseman Were alifuzu kwa nusu fainali ya mita 400 kuruka viunzi.

Share This Article