Tim Wanyonyi kugombea Ugavana Bungoma 2027

Martin Mwanje
1 Min Read
Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi akiwa na viongozi wengine wa Bungoma

Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi atagombea Ugavana wa Bungoma katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. 

Wanyonyi alimezea mate Ugavana wa Nairobi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 lakini akanyimwa nafasi ya kugombea wadhifa huo na chama chake cha ODM.

Badala yake, ODM ilimuunga mkono Polycarp Igathe aliyelambishwa sakafu na Gavana wa sasa Johnson Sakaja.

Kwenye mkutano uliofanyika katika hoteli ya Wanyangali viungani mwa mji wa Bungoma, viongozi mbalimbali wa kisiasa kutoka kaunti ya Bungoma walitangaza kumuunga mkono Wanyonyi kugombea wadhifa huo.

Miongoni mwa wanaosemekana kumuunga mkono Wanyonyi kugombea wadhifa huo ni wabunge tisa kutoka eneo hilo akiwemo mbunge wa Webuye Magharibi Dan Wanyama na Wawakilishi Wadi wapatao 62.

Hata hivyo, mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ambaye pia anataka kuwa Gavana wa Bungoma hakuhudhuria mkutano huo.

Kwenye hotuba yake, Wanyonyi aliwashukuru viongozi hao kwa kumuunga mkono na kutoa wito wa umoja katika kaunti yote ya Bungoma.

Aidha, aliwataka kutoegemea na chama chochote cha kisiasa kwa sasa.

Gavana wa sasa wa Bungoma ni Ken Lusaka ambaye kikatiba haruhusiwi kugombea wadhifa huo kwani atakuwa amehudumu mihula miwili kufikia wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

 

 

Share This Article