Tiketi za mechi ya tatu ya Kenya kundini A kuwania kombe la CHAN dhidi ya Morocco, Jumapili hii zimemalizika.
Mchuano huo umeratibiwa kuandaliwa kuanzia saa tisa alasiri katika uga wa kimataifa wa Kasarani.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa Morocco, walioishinda Angola kwa mabao 2-0 katika pambano la ufunguzi, huku ukiwa mchuano wa tatu kwa Kenya.
Kenya waliishinda DR Congo bao moja kwa bila Jumapili iliyopita, na watarejea uwanjani Kasarani kwa mchuano wa pili Alhamisi hii usiku dhidi ya Angola.
Tiketi za mzunguko zilikuwa zikiuzwa kwa shilingi 200 na shilingi 500 kwa zile za jukwaa kuu.