Tiketi za CHAN kuanza kuuzwa Jumanne ijayo

Tiketi za kawaida zitauzwa kwa shilingi 200, huku zile za VIP shilingi 500 na shilingi 1000 kwa zile za VVIP.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tiketi za makala ya nane ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN), zitaanza kuuzwa rasmi Jumanne ijayo, Julai 15.

Mwenyekiti wa kamati andalizi ya pamoja Nicholas Musonye alisema kuwa tiketi za kawaida zitauzwa kwa shilingi 200, huku zile za VIP shilingi 500 na shilingi 1000 kwa zile za VVIP.

Mataifa 19 yaliyotengwa katika makundi manne yatashiriki fainali hizo zitakazoandaliwa kati ya Agosti 2 na 30.

Tanzania watafungua michuano tarehe 2 mwezi ujao dhidi ya Burkina Faso katika uga wa Mkapa,  kabla ya Kenya kushikana mashati na mabingwa mara mbili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Agosti 3 kiwarani Kasarani.

Uganda itafungua ratiba ya kundi C Agosti 4 dhidi ya Algeria katika uchanjaa wa Nelson Mandela Namboole.

Share This Article