Tiketi za AFCON kuanza kuuzwa Jumamosi Septemba 27

Dismas Otuke
1 Min Read

Tiketi za fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Makala ya 35 zitakazoandaliwa nchini Morocco zitaanza kuuzwa kesho Jumamosi Septemba 27.

Morocco itaandaa Makala ya 35 ya kipute cha AFCON kati ya Disemba 21 mwaka huu na Januari 18 mwakani.

Mataifa 24 yatashiriki, yakiwemo 12 yaliyotwaa Kombe katika fainali 34 zilizopita.

Morocco itakuwa mwenyeji wa AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1988.

Jumla ya viwanja tisa vilivyo katika miji sita tofauti nchini vitatumika kwa patashika hiyo huku mechi ya ufunguzi na fainali zikisakatwa katika uga wa Prince Mullay Abdallah jijini Rabat.

Share This Article