Tanzania : Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Omar Nondo Apatikana

Francis Ngala
1 Min Read
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama Cha upinzani cha ACT Wazalendo Abdul Omar Nondo ambaye alitekwa na watu wasiojulikana Maeneo ya Stendi mbezi Magufuli wiki iliyopita amepatikana usiku wa kuamkia Leo Katika eneo la Coco beach akiwa ametelekezwa.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Tanzania DCP -David A. Misime inaeleza kuwa Disemba 1,2024 majira ya saa nne na nusu usiku Abdul Omary Nondo ambaye alikuwa anatafutwa Kwa kushirikiana na watu mbalimbali wakiwepo Viongozi wake wa Chama cha ACT Wazalendo alitelekezwa maeneo ya fukwe za Coco (Coco beach) Kinondoni Jijini Dar es Salaam na watu asiowafahamu.
Baada ya kutelekekezwa alisimamisha bodaboda na kumwelekeza amfikishe katika Ofisi za Chama chake zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ambapo walifika muda wa saa tano usiku ambapo alionana na Viongozi wake na alipelekwa Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Aidha jeshi la polisi limeongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kuwapata wahusika wa tukio hili ikiwa ni sambamba na kupata ukweli wa sababu au chanzo (motive) cha tukio hili ili hatua zingine za kisheria zichukuliwe.
Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.