Tanzania kuwasilisha bajeti ya shilingi trilioni 20

Baadhi ya vipa umbele kwenye bajeti ya Tanzania ni kukusanya shilingi trilioni 50.17, kutekeleza bajeti hiyo ya         mwaka mpya wa kifedha na kiwango cha shilingi trilioni 14.22, kikielekezwa kwa kulipa deni la serikali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Leo ni siku ya kusomwa kwa bajeti ya makadirio ya matumizi ya fedha ya mwaka 2025 na 2026, kwa mataifa mengi ya Afrika Mashariki.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Juni 5 mwaka huu, lillidhinisha bajeti ya shilingi trilioni 20.19, sawia na shilingi trilioni 1.25, za Kenya kwa matumizi ya fedha ya mwaka wa kuanzia Julai mosi  2025, hadi Juni 30 mwaka 2026.

Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kusoma rasmi bajeti hiyo bungeni leo alasiri.

Baadhi ya vipa umbele kwenye bajeti ya Tanzania ni kukusanya shilingi trilioni 50.17, kutekeleza bajeti hiyo ya         mwaka mpya wa kifedha na kiwango cha shilingi trilioni 14.22, kikielekezwa kwa kulipa deni la serikali.

Aidha,mamlaka ya ukusanyaji ushuru TRA, inadhamiria kukusanya ushuru wa shilingi trilioni 34.1,na kiwango kingine cha trilioni 1.07, kikitarajiwa kutoka kwa ruzuku.

Kati ya bajeti hiyo yote shilingi trilioni 19.43, zimetengewa gharama na matumizi ya kila siku huku shilingi biloni 557 kikitengewa kwa utekelezaji miradi ya Maendeleo ikiwemo miundombinu.

Share This Article