Wandaalizi wenza wa michuano ya CHAN Tanzania, Taifa Stars, watashuka uwanjani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa mechi ya tatu ya kundi B dhidi ya Madagascar kuanzia saa mbili usiku.
Tanzania wanaongoza kundi B kwa alama 6 baada ya kusajili ushindi dhidi ya Burkina Faso na Mauritania.
Madagascar watakuwa wakicheza mechi ya pili baada ya kutoka sare tasa na Mauritania.
Jamhuri ya Afrika ya Kati watachuana na Mauritania katika mechi ya kwanza ya leo kuanzia saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Mkapa.