Tanasha Donna kuondoa vitu alivyowekewa kwenye midomo

Hii ni baada yake kukosolewa na wengi mitandaoni kwa kubadili mwonekano wa midomo yake.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna hatimaye ametangaza kwamba ataondoa vitu alivyowekewa kwenye midomo baada ya kukosolewa na kushauriwa kufanya hivyo na wanamitandao.

Mwonekano wake mpya ulifahamika na wengi baada yake kuchapisha video akitoa ushauri hata ingawa alifanyiwa upasuaji huo wa kuimarisha midomo mwezi Aprili mwaka 2024.

Wengi wa wanaomfuatilia mitandaoni wanahisi kwamba midomo yake ilikuwa inavutia awali kabla ya upasuaji huo wa ujazo.

Dada wa Taifa nchini Tanzania Mange Kimambi naye hakuachwa nyuma katika kumkosoa Donna, akisema mpenzi huyo wa awali wa Diamond Platnumz ni mrembi kiasilia na kamwe hahitaji kujibadilisha.

Kabla ya hapo, Kimambi alisema kwamba alisoma maoni mengi ya wanaomfuatilia Tanasha kuhusu mabadiliko ya midomo yake na anawakosoa kwa kumfanyia mzaha na kumdhalilisha bila ya kumpa ushauri.

Aliendelea kumshauri kwamba aondoe ujazo huo wa midomo iwapo ni aina ya kuweza kuondolewa ili arejelee hali yake ya zamani na akajitolea hata kumlipia ada ya huduma hiyo.

“Kama ni ujazo tu ni tatizo dogo kutatua. Njoo haraka nikupeleka sehemu ya kuuyeyusha na Mange Kimambi app tutakupa offer ya kulipia huduma hiyo.” aliandika.

Zaidi ya hapo Mange Kimambi alisema kwa maoni yake, Donna ndiye mwanamke mrembo zaidi kati ya wanawake ambao mwanamuziki Diamond Platnumz amewahi kuwa na mahusiano nao.

Donna ana mtoto mmoja wa kiume na Platnumz.

Share This Article