Tamasha la Dax Vibes latupiliwa mbali

Vibez ambaye jina lake halisi ni Ivan Bugembe Sentamu, alitangaza habari hizo za kuvunja moyo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uganda Dax Vibez amepata pigo kubwa baada ya tamasha alilokuwa akiandaa kutupiliwa mbali ghafla.

Vibez ambaye jina lake halisi ni Ivan Bugembe Sentamu, alitangaza habari hizo za kuvunja moyo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

“Baada ya miezi tisa ya matangazo na uwekezaji, Hotel Africana imetupilia mbali tamasha langu. Sujui cha kufanya” aliandika msanii huyo ambaye ni kaka mdogo wa mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine.

Msanii huyo hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu hatua hiyo ambayo imelemaza tamasha lililokuwa liandaliwe Agosti 29, 2025.

Hii sio mara ya kwanza Hotel Africana inatupilia mbali tamasha ikikumbukwa kwamba mwanamuziki Alien Skin alikabiliwa na hali sawia mwezi Februari mwaka huu.

Share This Article