Takwimu za kipute cha CHAN baada ya mechi 38 za makundi

Wachezaji wengine 9 wamefumania nyavu mara mbili kila mmoja wakiwemo wakenya Austin Odhiambo na Ryan Ogam.

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya nane ya kindumbwendumbwe cha kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani (CHAN), kitaingia hatua ya robo fainali Ijumaa Agosti 22.

Kufikia sasa mechi 36 zimepigwa huku magoli 74 yakifungwa .

Wanandinga watatu;Thabiso Kutumela wa Afrika Kusini,Allan Okello wa Uganda na Oussama Lamlioui wa Morocco wanaongoza chati ya ufungaji magoli kwa mabao 3 kila mmoja.

Wachezaji wengine 9 wamefumania nyavu mara mbili kila mmoja wakiwemo Wakenya Austin Odhiambo na Ryan Ogam.

Jumla ya kadi 7 nyekundu zimetolewa huku Kenya ikiongoza kwa kuwa na kadi mbili nyekundu na kadi nyingine 119 za manjano.

 

Share This Article