Takwimu za kipute cha CHAN 2024

Mataifa ya Burkina Faso, Afrika ya Kati, Guinea na Nigeria yameaga mashindano.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya mechi 24 zimepigwa katika makala ya nane ya fainali za kombe la CHAN, yanayoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.

Magoli 51 yamefungwa huku wachezaji sita wakiwa wametikisa nyavu mara mbili kila mmoja.

Wao ni Clement Mzize wa Tanzania, Allan Okello wa Uganda, Thapiso Kutumela wa Afrika Kusini, Abdel Raouf wa Sudan na Kaporal wa Angola.

Mataifa ya Burkina Faso, Afrika ya Kati, Guinea na Nigeria yameaga mashindano.

Mechi za makundi zitakamilika Agosti 19, kabla ya mechi za robo fainali kusakatwa tarehe 22 na 23, ikifuatwa na nusu fainali Agosti 26 na 27.

Pambano la kuwania nafasi ya tatu na nne litapigwa Agosti 29, ikifuatwa na fainali Agosti 30.

Share This Article