Takwimu za CHAN 2024 kufikia sasa

Wachezaji wengine 25 wamefunga goli moja kila mmoja huku bao moja likiwa la kujifunga.

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya nane ya fainali za Kombe la CHAN yaling’a nanga Agosti 2, yakiandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Hadi sasa mechi 18 zimechezwa na magoli 32 kufungwa.

Wachezaji watatu wanaongoza kwa ufungaji mabao wakiwa na magoli 2 kila mmoja: Austin Odhiambo wa Kenya, Clement Mzize wa Tanzania na Kaporal wa Angola.

Wachezaji wengine 25 wamefunga goli moja kila mmoja huku bao moja likiwa la kujifunga.

Kenya inaongoza kundi A kwa pointi 7, ikifuatwa na Angola kwa alama 4 huku DRC na Morocco zikiwa na alama 3 kila moja na Zambia hawana alama.

Tanzania wanaongoza kundi B kwa alama 9, wakifuatwa na Mauritania kwa pointi 4, moja zaidi ya Burkina Faso, wakati Madagascar wakiwa na alama 1, huku Afrika ya Kati ikiburura mkia bila alama.

Algeria wanaongoza kundi C kwa pointi 4,moja Zaidi ya Uganda na Guinea walio katika nafasi za tatu nan ne nao Niger hawana pointi.

Senegal ni ya kwanza kundini D kwa alama 3, ikifuatwa na Congo na Sudan kwa alama 1 kila moja huku Nigeria ikiwa pasi na alama.

Share This Article