Takriban mashabiki 44,000 walihudhuria mechi ya Kenya dhidi ya Angola

Hali hii inaashiria shauku na ragba ya mashabiki wa Kenya kuiunga mkono timu ya taifa Harambee Stars ,kila inapocheza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Takriban mashabiki 44,900 walihudhuria mchuano wa kundi A kuwania kombe la CHAN kati ya Angola na Kenya, katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani Alhamisi usiku.

Idadi hiyo ni ya juu ikilinganishwa na uwanja huo unaoselehi mashabiki 48,000, baada ya kufanyiwa ukarabati.

Mechi zote ambazo zimechezwa uwanjani Kasarani kufikia sasa zimeshuhudia uuzaji tiketi ukimalizika takriban siku nne kabla ya siku ya mchezo.

Hali hii inaashiria shauku na ragba ya mashabiki wa Kenya kuiunga mkono timu ya taifa Harambee Stars ,kila inapocheza.

Share This Article