Balozi wa Marekani nchini Uturuki na Mjumbe Maalumu wa Syria Tom Barrack, amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkuu wa mamlaka ya mpito nchini Syria Ahmad al-Sharaa walikubaliana kusitisha mapigano kwa msaada wa Uturuki, Jordan na nchi jirani.
“Tunatoa wito kwa Druze, Bedouins, na Wasunni kuweka chini silaha zao na kufanya kazi na watu wengine walio wachache kujenga utambulisho mpya wa Syria,” Barrak alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Twitter.
Siku ya Jumatano, Israel ilianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Damascus, yakilenga majeshi ya serikali ya kusini, na kutaka waondoke, ikisema wakati huo “ililenga kulinda kuwalinda watu wa jamii ya Druze ya Syria.”
Damascus iliweka vikosi hivi kufuatia mapigano kati ya makabila ya Bedouin na wanamgambo wa Druze.