Susan Burns atwaa usimamizi wa Ubalozi wa Marekani nchini Kenya

Hadi uteuzi wake, Burns amekuwa Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Marekani nchini Vietnam kuanzia mwaka 2022.

Dismas Otuke
1 Min Read

Susan Burns emeshika hatamu za Msimamizi Mkuu wa Ubalozi wa Marekani nchini Kenya kumrithi Carla Benini ambaye muda wake umemalizika.

Burns anatwaa uongozi wa Ubalozi huo kutoka kwa Carla Benini, ambaye amehudumu afisini tangu mwaka 2023.

Hadi uteuzi wake, Burns amekuwa Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Marekani nchini Vietnam kuanzia mwaka 2022.

Pia amehudumu katika nyadhfa kadhaa katika mataifa ya Uganda, Poland, Brazil, Ubelgiji, Italia, India, Ghana, Taiwan na Nepal.

Share This Article