Surya Roshni yadhihirisha ubabe katika maonesho ya vifaa umeme barani Afrika

Maonesho hayo yalishirikisha kampuni kadhaa kutoka Afrika zinazojihusisha na vifaa vya umeme, mabomba.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya Roshni ya kutoka India inayofahamika kwa kuunda mabomba na vifaa vya umeme ilitamba wakati wa maonesho ya vifaa vya umeme yaliyoandaliwa katika ukumbi wa KICC, baina ya Julai 16 na 18 mwaka huu.

Maonesho hayo yalishirikisha kampuni kadhaa kutoka Afrika zinazojihusisha na vifaa vya umeme, mabomba.

Surya Roshni ilisaini mkataba wa kimkakati na kampuni ya Star Link ili kuongeza uwepo eneo la Mombasa na kote nchini.

Akizungumza katika maonesho hayo, Surya Roshni kupitia kwa mismamizi wake mkuu Vasumitra Pandey na msimamzii wake wa biashara za kimataifa Mr Sunil HR, walisema lengo lao ni kupanua soka lao nchini Kenya na pia ukanda wa Afrika mashariki kwa jumla.

“Surya Roshni, tunajitolea kuimarisha maisha ya Wakanya kwa kutengeneza bidhaa za kisasa na za bei nafuu,” akasema msemaji wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ilikariri kuendelea kushirikiana na wadau wengine humu nchini kuhakikisha vifaa vya kutoa mwangaza wa umeme vinapatikana kwa urahisi na pia vina thamani ya hali ya juu.

Share This Article