Msanii wa muziki nchini Uganda Diana Namukwaya Hajara maarufu kama Spice Diana amesema kamwe hawezi kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio.
Hata ingawa wasanii wengi wa kike wameamua kufuata mkondo huo kama njia ya kuimarisha mwonekano na kuongeza mvuto, Diana anasema ameridhika na mwili wake ulivyo.
Katika kikao na wanahabari msanii huyo alielezea kwamba kikubwa kinachomkwaza ni uchungu atakaohisi wakati wa kufanyiwa upasuaji huo na atakapokuwa katika kipindi cha kupona.
Mwimbaji huyo alitaja pia michoro kwenye ngozi almaarufu Tatoo na kutobolewa kwani vitu hivyo pia husababishia mtu uchungu.
Hata hivyo mwanadada huyo alisisitiza kwamba kila mmoja ana haki ya kufanya kinachomfurahisha na kwa sababu hiyo hana tatizo na yeyote ambaye amefanyiwa upasuaji huo.
“Nimeaibishwa mara kadhaa kutokana na mwonekano wango kwa kuwa namakalio madogo na niko na mchoro mmoja mdogo pekee kwenye mkono wangu kwa sababu naogopa uchungu.” Alisema Diana.
Kuhusu uhusiano kati yake na Sheebah Karungi, Spice Diana alikwepa swali hilo kutoka kwa wanahabari ambapo alijibu, “Ndugu yangu, ngoja niende msalani”.
Kumekuwa na uvumi unaosambaa kwamba wanamuziki hao wawili wa kike wa Uganda waliokuwa marafiki kwa sasa hawapatani, ugomvi wao ukiendelezwa na wafuasi wao mitandaoni.
Hata hivyo wadadisi wa masuala ya burudani nchini humo wanahisi kwamba ugomvi huo sio wa kweli ila unalenga tu kuwainua na kuuza kazi zao mitandaoni.