Simba wanusia fainali baada ya kuwang’ata Stellenbosch

Ni mara ya kwanza kwa 'wenye nchi hao' kufika hatua ya semi fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka nchini Tanzania bara Simba Sports Club,wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa bao moja kwa nunge Jumapili jioni katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.

Goli pekee na la ushindi kwa Wekundu wa Msimbazi, limepachikwa nyavuni na kiungo kutoka Ivory Coast Jean Charles Ahoua, katika dakika ya pili ya mazidadi kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilishuhudia pande zote zikifunga milango, na Simba kusajili ushindi huo mwembamba kufikia kipenga cha mwisho.

Simba watazuru Afrika Kusini kwa mchuano wa marudio tarehe 27 mwezi huu .

Ni mara ya kwanza kwa ‘wenye nchi hao’ kufika hatua ya semi fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

Share This Article