Simba wa Atlas wafungua CHAN kwa kishindo

Morocco wanaongoza kundi A kwa alama 3 sawa na Kenya iliyo ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara mbili wa kombe la CHAN Morocco, walianza kwa makeke kipute cha nane, baada ya kuwabwaga Angola magoli 2-0, katika mchuano wa kundi A, uliopigwa jana usiku uwanjani Nyayo.

Imad Riahi, aliwaweka Morocco uongozini kunako dakika ya 29, akiunganisha krosi ya nahodha Mohamed Hrimat.

Kipindi cha pili Angola walijizatiti kukomboa bao hilo lakini wakajisahau na kupigwa shambulizi moja la kushtukiza kunako dakika ya 81, na kusababisha beki Quinto kujifunga.

Morocco wanaongoza kundi A kwa alama 3 sawa na Kenya iliyo ya pili.

Baadaye saa mbili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Madagascar na Mauritania, waliambulia sare tasa katika mechi ya kundi B.

Kiungo wa Madagascar Andriamirado Andrianarimanana, alikuwa mchezaji wa kwanza kulishwa kadi nyekundu katika kipute cha mwaka huu.

Tanzania wanaongoza kundi B kwa alama 3, wakifuatwa na Madagascar na Mauritania kwa alama 1 kila moja.

Share This Article