Simba SC yaikwatua Gor Mahia mechi ya kirafiki

Mchuano huo ulikuwa wa maadhimisho ya siku ya Simba Dei.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa soka nchini Tanzania klabu ya Simba waliwashinda mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya, Gor Mahia, mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Jumatano jioni katika uwanja wa kitaifa wa Mkapa.

Mchuano huo ulikuwa wa maadhimisho ya siku ya Simba Dei.

Wekundu wa Msimbazi Simba walijipatia magoli yao kupitia kwa Abdulrazak Hamza na Steven Dese Mukwala katika kila kipindi.

Timu zote zilitumia mechi hiyo kama maandalizi ya mwisho kabla ya kungoa nanga kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kenya na ile ya Tanzania Bara.

Share This Article