Siku ya Mashujaa: Musalia Mudavadi amkaribisha Rais Kwale

Martin Mwanje
1 Min Read

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi ndiye aliyemkaribisha Rais William Ruto wakati wa sherehe za Siku ya Mashujaa zilizoandaliwa leo Jumapili katika kaunti ya Kwale. 

Hii inafuatia hatua ya Bunge la Seneti kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Gachagua ameugua na anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.

Rais Ruto amemteua Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu wake mpya.

Ingawa Prof. Kindiki alihudhuria sherehe hizo na kukaa mahali palipotengewa Naibu Rais, hakuhutubia hadhira.

Hata hivyo, uteuzi huo umepingwa mahakamani na kesi iliyowasilishwa na Gachagua kupinga uteuzi huo inatarajiwa kusikizwa na jopo la majaji watatu.

 

 

Share This Article