Shule ya Nakuru High yafungwa kufuatia vurumai za wanafunzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule ya upili ya Nakuru High imefungwa ghafla kufuatia vurumai za wanafunzi jana jioni.

Yamkini wanafunzi hao walianza kuzua vurumai jana jioni kabla ya saa tatu usiku na vurumai hizo kuendelea hadi usiku wa manane, kabla ya polisi kutuliza hali.

Wanafunzi hao waliteta uamuzi wa shule wa kuondoa chai ya saa nne asubuhi na kulazimishwa kunywa chai ya mkandaa kama staftahi.

Wanafunzi hao pia wanapinga kuanzishwa kwa malipo ya chakula kwa kutumia kadi badala ya pesa taslimu.

Kulingana na polisi, wanafunzi hao waliharibu mali ya shule, ikiwemo madarasa, mabweni na ofisi.

Share This Article