Ngarambe baina ya mabingwa mara 12 wa soka baina ya shule za upili nchini – Kakamega ( Green commandoes) na majirani wao Township imehairishwa kufuatia vurugu iliyotokea baada ya Kakamega kufunga bado katika muda wa ziada ambalo msaidizi wa muamuzi wa mchezo aliashiria kuwa lilikuwa la kuotea naye mwamuzi wa katikati akaashiria kuwa bao la haki.
Kutoelewana baina ya wawili hao kulisababisha mashabiki wenye ghadhabu kuingia ugani hivyo mchuano huo ukafutiliwa mbali na kuagiza marudio kufanyika hapo kesho kwenye uwanja usiojulikana na ambao huenda ukakosa mashabiki.
Mahasimu hao wa jadi walitoka sare ya sufuri kwenye muda wa kawaida licha ya Kakamega kuwatumbuiza kwa mchezo maridadi mashabiki waliofurika shuleni humo kutazama robo fainali ya kiwango cha kaunti ndogo ya Lurambi – kaunti ya Kakamega.
Maamuzi ya Marudio ya mchezo huo ni sawia na yale ya fainali ya kaunti ndogo jirani ya Shinyalu baina ya shule za wavulana za Mukumu na Shanderema.
Kwenye fainali hiyo, Mukumu waliongoza Kwa mabao mawili Kwa moja ila bao la pili la Mukumu likakataliwa kuwa la kuotea hivyo kusababisha hali ya tendabelua baina ya mashabiki wa timu hizo walioingia uwanjani. Mchezo huo ulihairishwa kwa siku kadhaa kisha ukarudiwa katika uga wa chuo cha ufundi cha Sigalagala chini ya Ulinzi mkali wa maafisa wa polisi.
Kama awali, timu hizo zilifungana bao kwa moja kisha katika muda wa kawaida na kuelekea katika mikwaju ya adhabu ambapo waakilishi wa eneo la Magharibi katika mashindano ya kitaifa ya mwaka wa 2023 – Shanderema walishinda 4-3 na kujikatia nafasi ya kushiriki daraja la Kaunti hapo