Shujaa na Lionesses zatua Marekani tayari kwa mchujo

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu za taifa za Kenya za wachezaji saba upande kwa wanaume Shujaa na ile ya wanawake Lionesses ziko mjini Los Angeles,Marekani tayari kwa mechi za kuwania kupandishwa na kushushwa ngazi baina ya tarehe 3 na 4 mwezi  huu.

Kenya imeratibiwa kupambana na Samoa Jumamosi hii kabla ya kuchuana na Ureno na  Marekani Jumapili.

Kenya Lionesses itafungua kampeini zake dhidi ya Uhispania Jumamosi kabla ya kukumbuna na Brazil  na Colombia.

 

Share This Article