Shughuli ya kuutazama mwili wa Raila inaendelea Mamboleo kisumu

Tom Mathinji
1 Min Read
Shughuli ya kutazama mwili wa Raila Odinga inaendelea katika uwanja wa Mamboleo kaunti ya Kisumu.

Shughuli ya kuutazama mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu hayati Raila Odinga, inaendelea katika uwanja wa Mamboleo kaunti ya Kisumu, na kuwapa wananchi fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

Zoezi hilo lilifunguliwa kwa maombi na viongozi wa kidini pamoja na wazee wa jamii ya wa Luo, saa nne kasoro robo Jumamosi asubuhi.

Usalama umeimarisha wananchi mmoja baada ya mwingine wakipiga foleni kuutazama mwili huo wa Raila, huku makundi ya dharura yakiwa tayari kutoa huduma za kwanza.

Baada ya shughuli hiyo kukamilika Jumamosi jioni, mwili huo baadaye utasafirishwa kwa ndege hadi nyumbani kwake bondo, ambako utakesha usiku kucha, kabla ya mazishi siku ya Jumapili.

Raila Odinga alifariki siku ya Jumatano akipokea matibabu nchini India.

Viongozi mbali mbali wa hapa nchini na wa kimataifa, wamemtaja Raila kuwa kiongozi aliyejitoa mhanga kulihutubia taifa lake na bara la Afrika kwa jumla.

Share This Article