Shilingi bilioni 14 za ufadhili wa elimu ya sekondari kutolewa hivi karibuni

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Elimu julius Ogamba.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba, amewahimza wakuu wa shule za umma za sekondari, kutowarudisha nyumbani wanafunzi kutokana na kucheleweshwa kutumwa kwa fedha za ufalidhili wa elimu kutoka kwa serikali.

Migos alisema kuwa wizara yake inashirikiana kwa karibu na Hazina Kuu, kuhakikisha nakisi ya shilingi bilioni 14 zinatumwa katika shule wiki ijayo.

Aliongeza kuwa wanafanya mikakati kuhakikisha ufadhili huo unatolewa mapema ili kuepusha changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa.

“Sio wazazi ambao hulipa karo ya shule, hulipwa kupitia fedha za ufadhili wa elimu na serikali. Tunajizatiti kuhakikisha fedha hizo zinatumwa shuleni wiki ijayo,” alisema waziri huyo.

Kuhusiana na mfumo mpya wa ufadhili wa masomo katika vyuo vikuu, waziri  Ogamba alisema jopo la kurejelea suala hilo lililobuniwa na rais lilikuwa likitia kitone cha mwisho kwenye ripoti yake.

Alisema jopo hilo lilikuwa limerejelea masuala kadhaa yaliyoibuliwa na wakenya na yale yaliyowasilishwa mahakamani ili kuhakikisha mfumo huo unawanufai wakenya wote.

Share This Article