Shabana FC wameandikisha rekodi mpya kwenye ligi kuu ya Kenya FK FPL, baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nairobi City Stars, Jumamosi uwanjani Machakos, wakienda mechi nane bila kushindwa.
Keith Imbali aliwaweka wageni Shabana uongozini katika dakika ya 52, kabla ya Darius Msagha, kutanua uongozi huo dakika ya 70 kwa bao la pili.
Shabana wanakalia nafasi ya nne ligini wakisalia na mechi sita kwa alama 46, pointi sita nyuma ya viongozi Police FC, waliotoka nyuma na kuwazaba Kenya Commercial Bank mabao 2-1.
AFC Leopards pia waliibuka kidedea 3-1 ugenini kwa Bidco United.
Awali, Kariobangi Sharks walipigwa 2-1 na Bandari FC, huku Posta Rangers wakiwalemea Murang’a Seal 3-2.