SHA yawataka Wakenya kujihadhari na walaghai

Wakenya kadhaa wameripotiwa kuporwa maelfu ya pesa na watu wanaojisingizia kuwa maafisa wa Mamlaka ya Afya ya Jamii, SHA.

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Mercy Mwangangi - Mkurugenzi Mtendaji wa SHA

Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) imetoa wito kwa Wakenya kujihadhari na watu ambao wanajisingizia kuwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo na kuwapora pesa. 

Watu kadhaa wameripotiwa kuporwa pesa na walaghai hao wanaodai wanaweza wakawasaidia kujiandikisha na SHA au kuharakisha kupokea huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo lakini baada ya kulipa ada fulani.

“Tafadhali fahamu kwamba wafanyakazi wa SHA kamwe huwa hawataki kulipwa pesa ili kutoa huduma, au kujua nambari yako ya siri ya M-Pesa. Ikiwa wewe au mtu unayemfahamu ameathirika, tunakuomba kupiga ripoti kwa polisi mara moja na kwa SHA kupitia namba yetu isiyotozwa malipo ya 147 au utume ujumbe kupitia baruapepe ambayo ni fraud@sha.go.co.ke,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SHA Dkt. Mercy Mwangangi kwenye taarifa.

Unaweza ukasoma maelezo zaidi kuhusu tahadhari ya SHA kuhusu walaghai kupitia taarifa ifuatayo:

Share This Article