SHA: Vituo vya afya vya umma vinavyowatoza wagonjwa ada vyaonywa

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto ametoa onyo kali kwa zahanati, vituo vya afya vya umma na hospitali za kaunti ndogo dhidi ya kuwatoza ada wagonjwa wanaotafuta huduma mbalimbali za matibabu katika taasisi hizo na kisha kurejea nyumbani.  

Ruto amesema taasisi hizo za matibabu zilitengewa shilingi bilioni 21 kwenye bajeti chini ya Mamlaka ya Afya ya Jamii, SHA, ili kuhakikisha dawa na huduma za matibabu zinazotolewa katika taasisi hizo za afya zinatolewa bila malipo.

Taasisi hizo ni za Level 2-Level 4.

“Kuna kaunti ambazo bado zinawatoza ada wagonjwa. Tafadhali komesha hilo,” alionya Ruto wakati akifungua Kongamano la Ugatuzi 2025.

Aliongeza kuwa taasisi yoyote itakayopatikana ikifanya hivyo itachukuliwa hatua kali.

Ruto sasa ametoa wito kwa Magavana kushirikiana na utawala wake bega kwa bega ili kuhakikisha huduma katika taasisi hizo zinatolewa bila malipo kwa wagonjwa.

 

Share This Article