Seville na Jefferson watawazwa mabingwa wa Dunia mita 100

Seville alinyanyakua dhahabu ya mita 100 kwa wanaume ikiwa taji ya kwanza ya Jamaica baada ya miaka 10, akiziparakasa kwa sekunde 9.77.

Dismas Otuke
1 Min Read

Oblique Seville wa Jamaica na Melissa Jefferson-Wooden  wa Marekani,ndio mabingwa wapya wa Dunia katika mbio za mita 100 kwenye mashindano yanayoendelea Tokyo,Japan.

Seville alinyanyakua dhahabu ya mita 100 kwa wanaume ikiwa taji ya kwanza ya Jamaica baada ya miaka 10, akiziparakasa kwa sekunde 9.77.

Mwenzake Kishane Thompson and Noah Lyles wa Marekani walinyakua fedha na shaba kwa sekunde 9.82, na sekunde 9.89 mtawalia.

Wooden ambaye hajashindwa mwaka huu alinyakua dhahabu ya wanawake kwa rekodi mpya ya mashindano ya sekunde 10.61, huku chipukizi wa Jamaica Tina Clayton, akishinda fedha kwa sekunde 10.76, naye bingwa wa Olimpiki Julien Alfred kutoka Saint Lucia akiridhia shaba.

Share This Article