Serikali yatoa ilani ya kubinafsisha kampuni ya KPC

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya ubinafsishaji mashirika ya umma imetoa ilani ya kubinafsisha kampuni ya Kenya Pipeline (KPC).

Ilani hiyo ilitolea jana Alhamisi baada ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri kufuatia ripoti ya uidhinishaji kutoka kwa bunge Oktoba mosi mwaka huu.

KPC kwa sasa inamilikiwa na serikali kwa asilimia 99 kupitia kwa Hazina Kuu huku wizara ya kawi ikimiliki asimilia 1 ya hisa za kampuni hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya ubinafsishaji  Faisal Abbas amesema hatua hiyo itawapa Wakenya fursa ya kumiliki hisa katika kampuni hiyo na mashirika mengine ya Kiserikali yanayofanya  vyema .

TAGGED:
Share This Article