Serikali yatenga shilingi bilioni 4.5 kugharimia matibabu

Dismas Otuke
0 Min Read

Serikali imetenga shilingi bilioni 4.5 kugharimia matibabu kufuatia hatua ya Shirika la Marekani la Misaada la Kimataifa (USAID) kusitisha msaada nchini.

Akizungumza leo nyumbani kwake Karen, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema shilingi bilioni 2 zimetengewa ununuzi wa dawa huku zingine bilioni 2.5 zikitengewa utoaji chanjo.

Aidha, Prof. Kindiki ameongeza kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 24.9, kufadhili miradi ya afya iliyokuwa ikifadhiliwa na serikali ya Marekani.

Share This Article