Viwanda 19 vya majani chai kote nchini vitanufaika na kitita cha shilingi bilioni 3.5, ili kuboresha miundombinu kama sehemu ya kuimarisha operesheni.
Hatua hiyo inalenga kushughulikia juhudi za kuhakikisha operesheni za viwada hivyo kama sehemu ya mpango mpana wa mageuzi yanayolenga sekta ya Majani Chai nchini.
Katibu wa kilimo Dkt. Kiprono Rono, alisema serikali inapanga kupunguza ushuru katika sekta ya Majani Chai, sawia na kupunguza ushuru wa vifaa vya kupakia.
Kulingana na Dkt. Rono, mageuzi yanayoendelea katika sekta ya Majani Chai, chai ya hapa nchini yatauzwa moja Kwa moja kupunguza gharama ya malipo na hivyo kumuongezea mkulima mapato.
“Tumetenga shilingi bilioni 3.5B kuimarisha miundomsingi katika viwanda 19 vya majani chai, kuhakikisha vinatimiza ubora unaohitajika,” alisema Dkt. Ronoh.
Dkt. Ronoh aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na wawakilishi wadi kaunti ya Kericho.
Alidokeza kuwa taifa hili litaandaa kongamano la kimataifa kuhusu Majani Chai Mwezi Oktoba mwaka huu, kwa lengo la kutafuta soko zaidi la Majani Chai kwa wakulima wa hapa nchini.