Serikali yatafakari kufuta madeni ya bilioni 6 ya Hustler Fund

Aidha, Mang’eni alitaka bunge kuidhinisha shilingi bilioni tano zaidi kugharamia hazina hiyo katika kipindi cha matumizi ya fedha mwaka 2025/2026.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali inatafakari kufutilia mbali deni la shilingi bilioni 6 zinazodaiwa Wakenya waliochukua mikopo ya hazina ya Hustler.

Katibu katika idara ya serikali inayosimamia wajasiria mali wadogo na wa kadri Susan Mang’eni, akiwa mbele ya kamati ya bunge jana Jumatano, alisema kuwa hawatakuwa na budi ila kufuta madeni hayo endapo juhudi za kuwashurutisha waliochukua mikopo kurejesha pesa zitafeli.

Aidha, Mang’eni alitaka bunge kuidhinisha shilingi bilioni tano zaidi kugharamia hazina hiyo katika kipindi cha matumizi ya fedha mwaka 2025/2026.

Share This Article