Wizara ya kilimo imetangaza kuongeza maradufu bei ya zao la miraa gredi ya kwanza na ya pili na pia aina ya Alele.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Kilimo na Ustawizaji wa Mifugo Mutahi Kagwe amesema kuwa bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa mara moja.
Kilo moja ya miraa gredi ya kwanza itakuwa ikinunuliwa kwa shilingi 1,300 kutoka 700 za awali, huku gredi ya pili ikipanda kutoka shilingi 350 hadi 700.
Kilo moja za miraa aina ya Alele sasa itakuwa ikiuzwa kwa shilingi 1000 kutoka 500 za awali.
Takriban watu milioni 4 nchini hutegemea zao la miraa huku watumizi wa zao hilo ikifikia milioni 10 kila siku kote duniani.