Serikali yaimarisha utoaji misaada kwa waathiriwa wa mafuriko Tana River

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali imeimarisha juhudi za utoaji misaada kwa waathiriwa wa mafuriko kaunti ya Tana River, huku ikisambaza misaada ya shilingi Milioni 60.

Maeneo yaliyonufaika na misaada hiyo ni pamoja na kaunti ndogo za Garsen, Bura na Galole.

Zoezi hilo ambalo lililoongozwa na Katibu wa mipango maalum Ismail Maalim,ni sehemu ya mpango mpana unaotekelezwa na asasi mbali mbali kuwasaidiw jamii dhidi ya madhara ya mafuriko.

“Zoezi hili ni sehemu ya mpango wa serikali ya taifa ya kuwasaidia walioathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni kuhakikisha wanapata bidhaa za kimsingi,” alisema Maalim.

Katibu huyo alidokeza kuwa kati ya familia 6,000 zilizoathiriwa na mafuriko, ni familia 2,000 ambazo tayari zimenufaika na msaada Kupitia mpango huo unaotekelezwa kwa pamoja kati ya serikali ya kaunti na Ile ya taifa.

Katibu Maalim alikuwa ameandamana na mwenzake wa sehemu za maeneo kame na maendeleo ya Kanda Harsame Kero, mbunge wa eneo hilo na viongozi wengine.

Share This Article