Serikali kuwianisha sheria za leba za humu nchini na zile za kimataifa

Mwadime alisema haya Ijumaa iliyopita alipohutubia kongamano la kimataifa la kila mwaka la Coalition for Social Justice, mjini Geneva Uswizi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imeanza mchakato wa kuwianisha mabadiliko ya sheria za wafanyikazi na zile za kimataifa kwa lengo la kuleta usawa kwa wote.

Katibu katika wizara ya wafanyikazi na maendelezo ya maarifa Shadrack Mwadime, amesisitiza kuwa serikali inatambua uhamasishaji wa haki za kibinadamu kama nguzo muhimu kwa kuafikia maendeleo endelevu.

Mwadime alisema haya Ijumaa iliyopita alipohutubia kongamano la kimataifa la kila mwaka la Coalition for Social Justice, mjini Geneva Uswizi.

Share This Article