Serikali kukabiliana na mashirika bandia ya ajira za ughaibuni

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetoa masharti makali kwa wamiliki wa kampuni za kuwasajili Wakenya wanaotaka kufanya kazi ughaibuni kama njia ya kuwaondoa matepeli katika sekta hiyo.

Katibu wa Wizara ya Leba Shadrack Mwadime alisema kuwa serikali itashirikiana na mataifa ya kigeni ili kuwakabili wamiliki wa mashirika yanayowalaghai Wakenya.

Mwadime alisema haya kwenye ziara yake ya kiserikali nchini Oman, akiongeza kuwa ushirikiano na mataifa ya kigeni utahakikisha kuwa ni mashirika halali pekee yanayopewa leseni za kuhudumu.

Katibu aliongeza kuwa Wakenya wengi wamelaghaiwa na mashirika bandia wanapotafuta ajira nje ya nchi.

Share This Article