Serikali imeongeza bajeti ya elimu hadi shilingi bilioni 702

Tom Mathinji
1 Min Read

Katika lengo la kuboresha mfumo wa elimu hapa nchini, Rais William Ruto amesema serikali imeongeza bajeti ya elimu kutoka shilingi bilioni 690 mwaka 2024, hadi shilingi bilioni 702 mwaka huu.

Kiongozi wa taifa alisema ufadhili huo umeimarisha miundo mbinu ya shule, kusaidia kuajiriwa wa walimu laki moja, na kupanua rasilimali za taasisi na vyuo vikuu.

Kulingana na Rais, lengo ni kuwapa wakenya ujuzi wa kufanikisha hadhi ya taifa hili kuwa taifa lililostawi duniani, kwa kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora.

Rais Ruto alisema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa shule ya upili ya wasichana ya Yusuf Haji huko Masalani, kaunti Garissa, ambako pia aliikabidhi shule hiyo basi jipya, na kuweka jiwe la msingi kwa awamu ya pili ya ujenzi wa shule hiyo.

Share This Article