Serikali imeanzisha upya mpango wa 4-K Club shuleni, asema Waziri Kagwe

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo Mutahi Kagwe.

Waziri wa Kilimo  Mutahi Kagwe amesema serikali itaanzisha upya mpango wa 4-K Club na kwa sasa mpango huo tayari umeanza kutekelezwa katika shule zote 31,218 za msingi za umma  kote nchini.

Kagwe alisema kufikia sasa,  watu  1,222 watakaotoa mafunzo wamepelekwa katika kaunti 36 huku shule  245 zikipewa vifaa vya kilimo cha kivungulio, vifaa vya unyunyuziaji mashamba maji,  mashine za kuangulia vifaranga pamoja na kujifunza kilimo kwa vitendo.

Akizungumza wakati alipoongoza uzinduzi wa mipango iliyoimarishwa ya 4-K Club  katika shule ya msingi ya Kihate, kaunti ya  Nyeri, Kagwe alisema mpango huo ni hatua ya serikali ya kutayarisha kizazi  kijacho  kuhusu biashara kupitia mafunzo ya kilimo kwa vitendo shuleni.

Alisema mipango hiyo sio ya shule pekee ila ni vituo vya ubunifu. Kagwe pia alisema wizara hiyo  inashinikiza kuwepo kwa mpango wa kidijitali wa 4-K club ili kuwawezesha   wanafunzi kupata ufahamu kuhusu kilimo kupitia teknolojia.

Alitoa wito kwa kaunti, sekta ya kibinafsi, walimu pamoja na wazazi kuunga mkono mpango huo.

Share This Article