Senegal kuanza kutetea kombe la CHAN leo dhidi ya Nigeria

Mchuano huo utang’oa nanga saa mbili usiku, ukitanguliwa na ule kati ya Congo na Sudan saa kumi na moja jioni.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa kombe la CHAN Senegal, ukipenda Teranga Lions, watashuka uwanjani Amaan kisiwani Zanzibar leo kwa mchuano wa ufunguzi dhidi ya Super Eagles kutoka Nigeria.

Mchuano huo utang’oa nanga saa mbili usiku, ukitanguliwa na ule kati ya Congo na Sudan saa kumi na moja jioni.

Simba wa Teranga na Super Eagles wanakutana leo kwa mara ya nane, Nigeria wakijivunia kushinda mechi 3, Senegal wakapata ushindi mmoja na mechi tatu zikamalizikia sare.

Share This Article